CHAUSIKU SAID,
MATUKIO DAIMA MWANZA.
Wakulima nchini wametakiwa kuachana na dhana ya kulima kimazoea na kutumia mbegu zisizo na ubora, badala yake wazingatie sheria, kanuni na taratibu za kilimo ili kupata matokeo yenye tija.
Wito huo umetolewa na Bwana Shamba Elekezi wa Kampuni ya ZAMSEED, Emmanuel Buseluka, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamhongolo, Jijini Mwanza.
ZAMSEED, inayojihusisha na uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za mahindi, imetaja mambo matatu muhimu kwa mkulima kufanikisha kilimo chenye tija: matumizi ya mbegu bora, lishe sahihi kwa mimea ikiwemo mbolea ya kupandia, kukuzia na kuzalishia, pamoja na udhibiti wa wadudu waharibifu.
Buseluka amesema Tanzania inazo aina tano za mbegu za ZAMSEED — 405, 520, 606, 638 na 721 — ambazo zimegawanywa katika makundi ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Kila aina inatofautiana kwa muda wa kukomaa na kiwango cha mavuno, ambapo ZAMSEED 721, inayofaa zaidi nyanda za juu kusini, inaweza kutoa hadi magunia 45 kwa hekari.
“Mkulima akifuata taratibu zote za kilimo na kutumia mbegu za ZAMSEED, atapata mavuno mengi yatakayomuongezea kipato na kumuinua kiuchumi,” amesema Buseluka.
0 Comments