NA MATUKIO DAIMA MEDIA KILOLO
WAJUMBE wa mkutano mkutano maalum wa kura za maoni za udiwani na ubunge kata ya Ruaha Mbuyuni jimbo la Kilolo wamekusanyika asubuhi ya Leo Agosti 4 kupiga kura zao.
Wajumbe hao leo watapiga kura ya diwani wa kata na mbunge baada ya kukamilika kwa mchakato wa wagombea hao kufika kujinadi.
Katika viwanja vya kupigia kura wagombea wote wa nafasi ya udiwani na mawakala upande wa wagombea ubunge wameshiriki kikamilifu kushuhudia Demokrasia hiyo ndani ya chama.
Matukio Daima Media imeshuhudia utulivu wa hali ya juu kwa wajumbe hao huku ulinzi ukiwa umeimarishwa eneo na mkutano.
0 Comments