Header Ads Widget

MASHINDANO YA NNE YA BUNIFU ZA SAYANSI YAFANYIKA LINDI


 Katika kuhakikisha wanafunzi katika shule za sekondari nchini wanaongeza hari na kukuza bunifu mbali mbali kupitia masomo ya sayansi Taasisi ya wanasansi chipukizi Tanzania (YST) imendesha mashindano mkoani Lindi ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kitaalam wa kubuni na tafiti za kisayansi zenye kuleta tija kwa jamii.

Hii ni mara ya nne kwa taasisi hiyo kufanya mashindano katika mkoa huo wa Lindi ikilenga  kuongeza chachu kwa wanafunzi wa shule za sekondari kupenda masomo ya sayansi.


Akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi katika mashindano hayo yaliyofanyika huko manispaa ya lindi mkuu wa wilaya hiyo bi. Victoria mwanziva aliwapongeza wanafunzi kwa kazi mzuri walizozifanya huku akiahidi serikali ya mkoa huo kuzitumia tafiti zao kwa kuziongezea thamani.

Naye mshauri Mkuu wa maswala ya kijamii kutoka kampuni ya shell Msomis Mmbena Amesema tangu mwaka 2013 kampuni hiyo ilipoanza  kusaidia Mradi wa wanasayasi chipukizi Tanzania na kwamba kumekuwa na mafanikio makubwa.

" Tumeweza kuona mafanikio mkubwa ambapo wanafunzi wameanza kuendelea kukuwa mwaka baada ya mwaka na niseme tu kuwa tumefarijika kuona shule zilizoshiriki pia zimeongezeka tangu mwaka 2013


Nabil karatela ni meneja mradi wa taasisi ya wanasayansi chipukizi Tanzania amesema toka mwaka 2011 yst ikiendesha mashindano hayo ambapo mpaka sasa umeonekana kuanza kuleta tija huku akieleza kuwa katika mashindano hayo ya nne shule tatu bora zitaenda kushindana jijini Dar es salaam mwezi Novemba

Amesema YST ni jukwaa ambalo linajitahidi kujenga utamaduni kwa vijana kwa kufanya utafiti na kugundua vitu vipya kiasi kwamba Hata wanavyoendelea kukua na kuendelea na masomo Yao utafiti uwe ni swala la kiutamaduni na lisiwe swala la kuelekezwa." alieleza Kamugisha 

Ameongeza kuwa lengo la kuyafanyia hayo yote ni kutengeneza kizazi ambacho kinaweza kuchukua jukumu la moja kwa moja kumaliza matatizo yanayowakabili Watu kuliko kusubiri Serikali ama wafadhiri kwa ajili ya kutatua matatizo hayo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI