Header Ads Widget

TAIFA STARS YAENDELEA UBABE CHAN

Na Leonard johnson

Timu ya taifa nchini Tanzania [Taifa stars] imeendeleza ubabe katika michuano  ya CHAN 2024 baada ya kushinda goli 1-0 dhidi ya Mauritania  katika mchezo ulio chezwa hapo jana uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam .

Ikumbukwe kuwa Tanzania ipo kundi B  akiwa kinara kwa alama 6 , Anafuatiwa na burkinafaso  2 , timu zingine ni mauritania 1,na central Africa Republic 1,alama hizo Taifa stars imezipata baada ya kugawa Dozi kwa Burkinafaso 2-0,na 1-0 dhidi ya Mauritani .

Hatahivyo,katika mashindano hayo licha ya Ushindi ambao Tanzania imekuwa ikiupata imeendelea kuonyesha ubora wake kwa kutoa wachezaji bora wa mechi na katika mechi ya ufunguzi wa michuano hii, mchezaji bora wa mechi alichukua Kiungo mshambuliaji Feisal Salum ,na mechi ya pili  ya Tanzania dhidi ya Mauritania Mudathiri Yahya ameibuka mchezaji bora .

Sanjali na hayo ,katika ushindi ambao wameupata wamefanikiwa kujivunia kitita cha pesa shilingi mil 55,ambapo mil 10 ni hamasa ya goli la Mama ,Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, mil 20 kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila na mil 25 kutoka kwa mdau wa michezo.

Hivyo Timu ya Taifa Stars  kwasasa imeweka imani kubwa  kufuzu kwenda hatua ya 16 Bora ya michuano hii ,ikiwa imebakiza michezo miwili dhidi ya Madagascar na central Africa Republic ,Tanzania inahitaji droo moja tu kufuzu kwenda 16 Bora. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI