SERIKALI ya Mtaa wa Mbwamaji uliopo Kata ya Somangira Manispaa ya Kigamboni kupitia mkutano wake na Wananchi wa Mtaa huo, Agosti 29, 2025 wameomba juhudi za haraka ujenzi wa shule ya Msingi katika Mtaa huo ili kupunguza kero kwa Wanafunzi wanaofuata shule mbali na Mtaa huo.
Yohanne Luhemeja 'Maziku' ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo wa Mbwamaji, amesema awali shule ya Msingi Gezaulole ilikuwa katika Mtaa huo wa Mbwamaji na baadae ilihamishwa kupelekwa Mtaa Kizani.
"Mtaa wa Mbwamaji ina watoto Wanafunzi zaidi 750 waliokuwa wakisoma hapo na sasa wanafuata huduma hiyo ya shule katika eneo la Kizani ambapo ni mbali.
Hata hivyo, tunashukuru Serikali kwa kupokea jambo hili na tayari wametenga bajeti ya awali Milioni 200 itakayotoka kwa awamu za ujenzi wa shule yetu mpya ya Msingi katika Mtaa wetu na tunaamini itaondoa kero kwa watoto kwenda umbali mrefu" Amesema Maziku.
Na kuongeza kuwa: Wananchi wamekuwa wakiomba kuharakishwa kwa ujenzi wa shule ndani ya Mtaa huo hivyo kwa hatua za sasa kuna matumaini makubwa huku akiomba Wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali.
Kikao hicho cha kikanuni ni cha tatu kwa Serikali ya Mtaa huo wa Mbwamaji chini ya Mwenyekiti kukutana na Wananchi wake ambapo pia mambo mbali mbali waliweza kujadili ikiwemo suala la Ulinzi na Usalama, Elimu, pamoja na Miundombinu ya Mtaa huo.










0 Comments