.
NA MATUKIO DAIMA MEDIA
DODOMA; MGOMBEA urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mpinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza wake, Dk Emmanuel Nchimbi wanatarajia kesho kuchukua fomu ya urais kwenye ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)
Hatua hiyo imekuja baada ya jana INEC kutoa ratiba inayoonesha kuwa wagombea urais na makamu wa rais wa Tanzania kutoka vyama mbalimbali vya siasa wanatarajiwa kuchukua fomu kuanzia Agosti 9, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari alasiri hii mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi, Mafunzo na Uenezi wa CCM, CPA Amos Makalla, amesema Dk Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM atachukua fomu hizo ofisi za INEC jijini Dodoma.
Ratiba inaonesha kuwa mwisho wa kuchukua fomu kwa wagombea hao itakuwa Agosti 27, 2025, wakati kwa wanaowania ubunge na udiwani wataanza kuchukua fomu Agosti 14, 2025 hadi Agosti 27 mwaka huu. Uteuzi kwa wagombea wote itakuwa Agosti 27, 2025.
0 Comments