Header Ads Widget

REA KUANZA USAMBAZAJI NA UUZAJI WA MAJIKO BANIFU MKOANI RUKWA


Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Msalika Makungu, leo Agosti 27, 2025, ametembelewa na ugeni kutoka Wakala wa Nishati Vijijini  katika ofisi yake iliyopo katika mtaa wa  1 Barabara ya mkoani mkoa wa  Rukwa..

Wakala huo ambao unajishughulisha na usambazaji wa nishati vijijini  kwenye  mikoa yote ya Tanzania Bara, kwa sasa umekuja na mradi mwingine mpya wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku katika mikoa yote ya Tanzania Bara.

Akizingumza wakati wa utoaji wa  taarifa ya mradi, Mhandisi Kelvin Tarimo amesema, Lengo la kumtembelea Katibu Tawala wa Mkoa ni kutambulisha mradi huo wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku wenye thamani ya zaidi ya Milioni  291.3, ambapo kwa mkoa wa Rukwa  mradi utatekelezwa kwenye wilaya tatu  ambazo ni wilaya ya Kalambo, Sumbawanga na Nkasi na  kila wilaya itapata idadi ya majiko banifu 1,698.


Akitoa ufafanuzi juu ya lengo la mradi huo hapa Rukwa, mhandisi Tarimo, amesema;

“Mradi unalenga kusambaza majiko banifu ili kukuza upatikanaji wa Nishati safi na endelevu, kupanua usambazaji wa Nishati mbadala katika maeneo ya vijijini na hivyo kuhamasisha matumizi ya teknolojia safi kupitia teknolojia za kisasa  na bora za kupikia.

Mhandisi Tarimo ameendelea kwa kusema, asilimia 82 ya nishati kuu inayotumika nchini inatokana na tungamoto (biamass) kwa matumizi ya kupikia, inakadiriwa kuwa takribani asilimia 90 ya kaya nchini hutumia nishati ya kuni na mkaa kama nishati kuu ya kupikia ambapo matumizi ya kuni ni aslimia 63.5 na mkaa ni asilimia 26.2


Kupitia utafiti uliofanyika 2016 unakadiria kuwa takribani watu 33,024 hufariki kabla ya wakati kila mwaka hii ni sawa na asilimia 8.49 ya vifo vyote nchini Tanzania, kutokana na magonjwa ambayo yanachangiwa na uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba wakati wa upikaji kwa kutumia nishati isiyo safi na salama.

Kwa kutambua hilo, serikali kupitia wakala wa nishati vijijini umeandaa mpango wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku yenye ufanisi mkubwa katika utumiaji wake. 

Kwa mkoa wa Rukwa, zoezi la usambazaji na uuzaji wa majiko banifu utafanywa na mtoa huduma kampuni ya Greenway Grameen Infra Pvt Limited na ECOMANA Tanzania Limited ambapo jumla ya majiko banifu 5,094 yatauzwa kwa wananchi kwa bei ya ruzuku.

Gharama ya jiko moja ni TZS 71,500 lakini serikali imetoa ruzuku ya asilimia 80 hivyo mwananchi atanunua jiko kwa gharama ya TZS 14,300.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, ameishukuru REA kwa kuendelea kutekeleza kwa vitendo mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ili mpaka ifikapo 2034 basi asilimia 80 au zaidi ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia





 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI