Header Ads Widget

PAMBA YATAJWA KUINUA UCHUMI WA TAIFA ,WAKULIMA WATAKIWA KULIMA KWA MAARIFA.


Na chausiku said 

Matukio Daima Mwanza.

Wakulima wa zao la pamba Kanda ya Ziwa na Mikoa yote inayolima pamba wametajwa kunufaika kwa kiasi kikubwa na soko la zao hilo kwa kuwa hakuna mkulima aliyekosa kuuza pamba kwa msimu huu wa mwaka 2025.

Hayo yamebainishwa na Afisa Kilimo kutoka Bodi ya Pamba, Sharifa Salumu, wakati akizungumza na waandishi wa habari Agosti 4, 2025 katika Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nyamhongolo jijini Mwanza.


Afisa kilimo bodi ya pamba Sharifa Salumu akionyesha mfano pamba safi iliyovunwa kwa kuzingatia kanuni/taratibu za uvunaji wa pamba                                                                                                                                                                     

Amesema kuwa wanunuzi wanaendelea kununua pamba kwa wingi tangu msimu ulipoanza hadi sasa kwa bei elekezi ya Serikali ya shilingi 1,150 hadi 1,200 kwa kilo.

Sharifa amewataka wananchi kufika katika mabanda ya Bodi ya Pamba yaliyopo katika mikoa ya Mwanza, Simiyu (Nyakabindi) na Tabora (Ipuli) ili kujifunza kuhusu mnyororo wa thamani wa zao hilo kuanzia shambani hadi kufikia kuwa nguo.

Afisa kilimo bodi ya pamba Sharifa Salumu akimuonesha mteja aliyefika katika banda hilo namna ya kusoma mzani na kupata risiti yake.

Aidha amefafanua kuwa mkulima anayefuata kanuni bora za kilimo ana uwezo wa kuvuna kati ya kilo 1,000 hadi 2,700 kama ambavyo mkulima kutoka Chato alivyolima na kuvuna kilo nyingi.

Aidha, amesema pamba ni zao la kimkakati ambalo Serikali inalitegemea kwa ajili ya kupata fedha za kigeni, hivyo wakulima wanapaswa kulima kwa maarifa na bidii ili kupata tija.

Afisa kilimo bodi ya pamba Sharifa Salum akionyesha mfano wa ndege nyuki namna ambavyo inatumika kupulizia dawa katika mashamba.

Amesema kuwa mbegu mpya ya UKM08 imeboreshwa kwa kuondolewa uchafu, kupunguzwa nyuzi na kuwekwa dawa ya kuzuia wadudu kabla ya kuoteshwa.

"Ikiwa mbegu hiyo itaoteshwa kwa nafasi sahihi ya sentimita 60 kwa 60 na 30 kwa 30, mkulima anaweza kuvuna kilo 1,000 hadi 1,200 kwa hekari"Alisema Sharifa.

Sharifa amesema kuwa msimu uliopita wamekuwa na matrekita 400 ambayo yamewalimia mkulima wa pamba Kwa hekari moja Kwa sh 35 bei hiyo ikiwa ni pungufu ukilinagamisha na matrekta y watu  binafsi ambayo yamekuwa yakiwalimia wakulima hao Kwa hekari moja Kwa sh 60.
afisa Kilimo Wilaya ya Geita Robert Matondwa wa pili kutoka kushoto akiwa na wakulima wa zao la pamba katika shamba darasa la zao hilo

" Kwa hiyo sisi kama bodi ya pamba msimu huu tutaongeza matrekita mengine 300 hivyo  basi tunaweza kuwa na matrekta zaidi ya 500 Kwa ajili ya kuwalimia mkulima ili waweze mkulima maeneo kubwa Kwa wakati mfupi" Alisema Sharifa.

Mkulima wa zao la pamba, Mussa Philipo, aliyefika katika banda hilo kuhakiki usahihi wa mzani aliotumia kuuza pamba, amesema kuwa mzani huo haukuwa na changamoto yoyote.

Katika banda hilo, Bodi ya Pamba inatoa elimu juu ya matumizi ya mbolea hai, mizani janja ya kidijitali, matumizi ya droni na matrekta ya kisasa kwa ajili ya kupulizia na kulimia mashamba makubwa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI