Header Ads Widget

NCAA YAPOKEA MAHEMA 10 KUTOKA CARIBBEAN NAPLES ZOO TANZANIA.

 



Na,Jusline Marco:Arusha                                                                                                                              

Taasisi ya Caribbean Naples Zoo Tanzania kutoka nchini Marekani imetoa msaada wa mahema 10 kwa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kuimarisha shughuli za uhifadhi wa faru weupe na wanyama wengine waliopo katika eneo la urithi wa dunia la Ngorongoro.                                                                                                                                                                        

Mwakilishi wa taasisi hiyo Albert Mollel akizungumza wakati akikabidhi mahema hayo amesema kuwa wametoa msaada wa vitendea kazi hivyo ikiwa ni muendelezo wa ishirikiano katika kuimarisha ulinzi na uhifadhi endelevu wa rasilimali za wanyama pori adimu na waliopo hatarini kutoweka hususani faru.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Kamishna wa Uhifadhi NCAA Bw. Abdul-Razaq Badru ameishukuru taasisi hiyo kwa masaada huo na kusisitiza kuwa vifaa hivyo vitawawezesha askari wa uhifadhi kufanya kazi kwa ufanisi zaidi katika ulinzi wa fari na wanyama wengine waliopo kwenye hifadhini ya Ngorongoro.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi(Idara ya maendeleo ya Jamii NCAA ) Grolia Bideberi akielezea huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo kwa jamii iliuoko ndani ya hifadhi ya Ngorongoro amesema ni pamoja na utoaji wa elimu juu ya uhifadhi shirikishi, utunzaji wa mazingira,sambamba na uanzishwaji wa vikundi vya kiuchumi kwa wananchi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI