Header Ads Widget

MINADA YOTE NCHINI KUTUMIA NISHATI SAFI YA KUPIKIA - DKT. BITEKO


 “ Kama mnavyofahamu, Mhe. Rais alitoa maelekezo kuwa watanzania asilimia 80 ifikapo 2034 watumie nishati safi ya kupikia, maelekezo yake yanaendelea kutekelezwa, tulianza na taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100  kuondoa matumizi ya kuni na mkaa ikiwemo  magereza yote nchini, shule za Sekondari , vyuo na taasisi nyinginezo lakini moja ya maeneo yaliyobaki ni pamoja na minada ambayo inahudumia watu wengi.” Amesema Dkt.Biteko


Safari hiyo ya kuhakikisha minada yote nchini inatumia nishati safi ya kupikia, imeanzia katika Mnada wa Msalato jijini Dodoma ambapo tarehe 21 Agosti 2025, Dkt. Biteko amegawa majiko banifu kwa Mamalishe takriban 27 wanaohudumu katika mnada huo pamoja na majiko ya kuchomea nyama.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI