Polisi nchini New Zealand wamemkamata mwanamke mmoja baada ya msichana wa miaka miwili kupatikana akiwa hai ndani ya sanduku lake.
Kisa hicho kilitokea kaskazini mwa New Zealand siku ya Jumapili wakati basi lililokuwa likisafiri kutoka Whangarei kwenda Auckland liliposimama kwenye kituo cha basi katika mji mdogo.
Polisi walisema dereva wa basi alimtilia shaka mwanamke huyo alipoomba kupata eneo la kuhifadhia mzigo wake chini ya basi wakati wa mapumziko wakati wa safari.
"Dereva aliingiwa na wasiwasi alipoona begi la mwanamke likisogea. Alipofungua sanduku hilo, alimuona msichana wa miaka miwili ndani," polisi wa New Zealand walisema katika taarifa.
Kulingana na mamlaka, msichana huyo alikuwa amevaa nepi pekee na alikuwa amejifungiwa ndani ya sanduku kwa takriban saa moja.
Bado haijulikani iwapo kuna uhusiano wowote kati ya msichana huyo na mwanamke aliyemfungia kwenye sandugu. Mshtakiwa atafikishwa katika mahakama ya eneo hilo siku ya Jumatatu.
Kwa mujibu wa polisi, "Mwili wa msichana huyo ulikuwa wa joto sana lakini hakuwa amejeruhiwa kimwili."
Polisi wanasema baada ya tukio hilo, msichana huyo alipelekwa hospitalini ambako alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
"Tungependa kumpongeza dereva wa basi, ambaye aliona kuna kitu kibaya na kuchukua hatua mara moja, vinginevyo matokeo yangekuwa mabaya zaidi," polisi
0 Comments