Na mwandishi wetu
Mkutano na waandishi wa habari uliopangwa kufanyika leo saa 7 mchana na Mgombea wa Urais kwa kiteki ya Chama Cha ACT-Wazalendo Luhaga Mpina umeahirishwa kutokana na mzungumzaji kuendelea na usikilizaji wa kesi mahakamani.
Chama cha ACT-Wazalendo kupitia Afisa Habari wake, Abdallah Khamis, kimeomba radhi kwa usumbufu uliosababishwa na kimeeleza kuwa taarifa nyingine kuhusu tarehe mpya ya mkutano huo itatolewa baadaye.
0 Comments