Header Ads Widget

MISA TAN na TBL WANOGESHA USIKU WA WAANDISHI WA HABARI.


 Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini Mwa Afrika, Tawil la Tanzania ( MISA Tanzania) imeishukuru Kampuni ya  Bia ya  Tanzania Breweries Limited (TBL) Kwa kuwa karibu wa WAANDISHI  wa habari Tanzania.

Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bwana Edwin Soko amesema hayo wakati wa ufunguzi wa hafla ya jioni Kwa wanachama wa MISA Tanzania iliyofanyika kwenye ukumbi wa PSSSF Commercial Complex, Dar es salaam.

Kampuni ya Bia ya TBL  iliahirikiana na MISA Tanzania kwenye kuandaa hafla hiyo muhimu Kwa wanachama wa MISA.

Hafla hiyo ililenga kuwaleta pamoja  wanachama wote wa MISA toka Mikoa mbalimbali  Ili kuburudika baada ya mkutano wao Maalumu uliofanyika jana Agosti 14 , 2025.

Bwana Soko aliongeza kuwa TBL ni wadau wa muhimu wa MISA Tanzania na MISA itaendelea kufanya kazi Kwa karibu na TBL.

Pia Soko aliushukuru uongozi wote wa TBL na menejimenti na wafanyakazi wote na kutaka Kampuni nyingine Nchini kuiga mfano wa TBL kwenye kuwa karibu na Vyombo vya habari.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI