Header Ads Widget

MFUNGWA ALIYEFUNGWA JELA MIAKA 10 KWA KUBAKA ABAKA TENA GEREZANI..

 


MFUNGWA Emmanuel Magede aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10 na Mahakama nchini Zimbambwe  kwa kumbaka mtoto mdogo amekutwa na hatia ya kumbaka mfungwa mwenzake aliyekuwa anaoga wakiwa gerezani.


Mwendesha mashtaka, Loveit Muringwa alithibitisha kuwa Julai 23, 2025, Magede alitenda kosa hilo kwa mfungwa mwenzake wakati alipokuwa anaoga.

Mashahidi Tinashe Muyambo na Antony Chambarambanda ambao pia ni wafungwa katika gereza hilo, walidai kumwona Magede akiingia bafuni na kushuhudia tukio hilo la mfungwa huyo akifanya tendo la ndoa la kinyume na maumbile na mlalamikaji bafuni.

Hakimu Letwin Rwodzia alimuongezea hukumu kwa kuzingatia maumivu aliyopata mlalamikaji, mahakama ilisisitiza kuwa mashambulizi ya kijinsia yenye ukatili hayakubaliki.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI