Header Ads Widget

MEZA YA MAGAZETI LEO J4 AGOSTI 12/2025:CCM KUKUSANYA BILIONI 100 ZA KAMPENI,MAZISHI YA MTANGAZAJI TEMIGUNGA MAHONDO KUFANYIKA LEO KATA YA IFUNDA IRINGA ,RC IRINGA , DC IRINGA ,WAZIRI LUKUVI WATOA POLE

Mwili wa mwandishi wa habari Temigunga Mahondo umewasili jana junatatu kutoka Hospital ya Benjamin Mkapa Dodoma na kupokelewa na mamia ya wananchi wa Iringa wakiongozwa na waanahabari wenzake. 

 Huku viongozi mbali mbali wa mkoa wa Iringa wakifika kutoa salamu za pole na wengine wakituma salama hizo.

 Toka juzi Jumapili ulipotokea Msiba huo mkuu wa Wilaya ya Iringa Benjamin Sitta na mkuu wa mkoa wa Iringa Kheri James wamekuwa bega kwa bega na waombolezaji hao kufika nyumbani na kusaidia kamati ya mazishi inayoongozwa na mwenyekiti Victor Chakudika na katibu wake Ally Msigwa kuweka maandalizi vizuri katika mazishi hayo. 

 Huku waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu Sera na uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi ambae anatoka mkoa wa Iringa na akituma salamu za rambi rambi kwa wafiwa. 

 Lukuvi alisema Temigunga alikuwa msaada mkubwa kwenye tasnia ya habari na wakati wote akiwa mbunge wa Ismani Temigunga akiwa mtangazaji wa kituo cha Radio Country fm alikuwa akifanya kazi ya kueneza habari njema za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi jimbo la Ismani.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI