Header Ads Widget

MDAU DANY MANJIWA AMLILIA TEMIGUNGA MAHONDO

Ilikuwa mwaka 2003, kabla sijamfahamu kwa sura wala kuikariri sauti yake, tayari nilikuwa nimeshasimuliwa kuhusu upendo wake mkubwa kwa wenzake pale Redio County FM. Rafiki yangu kipenzi, marehemu George Ndabagoye, alinieleza hivi, nanukuu:

“Kaka, nimepata kazi pale Redio County FM kwa kaka Gerry Kindole. Kuna mtu anaitwa Temigunga Mahondo, ni mtu na nusu! Ananifundisha mengi hadi najiona mtangazaji mkubwa, wakati ndio kwanza naanza.”

Mwisho wa kunukuu. Huyo ndiye Temigunga, ambaye alipenda tumuite Temmy G. Alikuwa akitayarisha vipindi, kutengeneza matangazo, na wakati mwingine akitunga midundo ya muziki kwa vijana waliomuomba awasaidie ili watoke kimuziki.

Leo nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha rafiki mwema Temmy G, kilichotokea alfajiri. Natamani ungeamka uone namna rafiki zako wanavyokupost na kukukumbuka kwa upendo mkubwa. Inaumiza sana… Mungu huwachukua watu wema mapema, lakini mapenzi yake yatimizwe.

Najua umelala usingizi wa milele. Namuomba Mungu apokee roho yako, kaka mwenye moyo wa upendo kwa kila mtu. Pole kwa familia ya Mahondo, pole kwa tasnia ya habari.

Utakapokutana na Ndole huko, msalimie. Siku nisiyoijua tutaonana tena katika ile asubuhi njema na iliyo kuu. Tunamshukuru Mungu kwa maisha yako hapa duniani.

#WhatALoss

Anaandika Dany Manjiwa kutoka Kihesa Iringa 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI