Header Ads Widget

MAVUNDE ATOA AGIZO KWA SOTTA MINING KUKAMILISHA NYUMBA ZA WANANCHI WALIOPISHA MRADI WA DHAHABU SENGEREMA

Anthony Mavunde wa pili kutoka kulia akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Perseus nchini Tanzania, Lee Anne de Bruin wakisaini mkataba wa nyongeza kati ya Serikali na Kampuni ya Nyanzaga Mining Company Limited kwa ajili ya uchimbaji mkubwa wa dhahabu kupitia kampuni ya ubia ya Sotta Mining Corporation Limited

 Na chausiku said 

Matukio Daima Mwanza.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ameutaka uongozi wa Kampuni ya Sotta Mining kuhakikisha unakamilisha ujenzi wa nyumba 262 za wananchi waliopisha mradi wa uchimbaji dhahabu katika kijiji cha Sotta, wilaya ya  Sengerema, ifikapo Oktoba 31 mwaka huu, kama makubaliano yanavyoelekeza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, akizungumza katika Hafla hiyo asema mradi huo unaotarajiwa kugharimu zaidi ya dola milioni 500 utaleta mabadiliko ya kiuchumi


Agizo hilo amelitoa Jana Agosti 20, 2025 wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa nyongeza kati ya Serikali na Kampuni ya Nyanzaga Mining Company Limited kwa ajili ya uchimbaji mkubwa wa dhahabu kupitia kampuni ya ubia ya Sotta Mining Corporation Limited.

Mavunde amesema kuwa  hadi sasa nyumba 129 kati ya 262 zilizopangwa zimekamilika, na Serikali itahakikisha wananchi wananufaika na mradi huo kwa kupewa kipaumbele cha ajira na fursa za biashara.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Perseus nchini Tanzania, Lee Anne de Bruin akizungumza katika Hafla hiyo kusaini mkataba

Alibainisha kuwa mradi huo wenye thamani ya zaidi ya trilioni moja unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa taifa ikiwemo ajira, mapato ya serikali na ushiriki wa Watanzania katika utoaji huduma na biashara.

“Kama Wizara ya Madini tutahakikisha wazawa wanashirikishwa kwa kiwango kikubwa, mwekezaji kushirikiana na jamii, na miradi ya kijamii kupewa kipaumbele,” alisema.
Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano, Sifuni Mchome, akizungumza katika Hafla hiyo kusaini mkataba amesema Serikali imeongeza hisa zake zisizofifishwa kutoka asiliia 16 hadi 20,m

Aidha, Mavunde alibainisha kuwa mchango wa sekta ya madini katika pato la taifa umefikia asilimia 10.1 mwaka 2024, ikizidi lengo lililowekwa la kufikia kiwango hicho mwaka 2025.                                  
Kwa mujibu wa takwimu, maduhuli yaliyokusanywa na sekta hiyo yameongezeka kutoka bilioni 162 mwaka 2015/2016 hadi kufikia trilioni 1.7 Juni 30, 2025, sawa na asilimia 113 ya lengo.                                                                                                                                                                                    


Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, alisema Serikali inamiliki asilimia 20 ya hisa katika mradi huo na inatarajia kupata zaidi ya shilingi milioni 400 za gawio katika kipindi cha miaka 11 ya mradi.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Janet Lekashingo, alibainisha kuwa mradi huo ni kielelezo cha utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha sekta ya madini inachangia ipasavyo kwenye pato la taifa na maendeleo ya wananchi.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Janet Lekashingo, akizungumza katika hafla hiyo namna sekta ya madini itavyochangia Pato la Taifa.

Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, alisema Serikali inamiliki asilimia 20 ya hisa katika mradi huo na inatarajia kupata zaidi ya shilingi milioni 400 za gawio katika kipindi cha miaka 11 ya mradi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Janet Lekashingo, alibainisha kuwa mradi huo ni kielelezo cha utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha sekta ya madini inachangia ipasavyo kwenye pato la taifa na maendeleo ya wananchi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano, Sifuni Mchome, aliongeza kuwa kupitia mazungumzo na makubaliano mapya, Serikali imeongeza hisa zake zisizofifishwa kutoka asilimia 16 hadi 20, na kufikia mgawanyo wa 20% kwa Serikali na 80% kwa Nyanzaga Mining Company Limited.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, alisema mradi huo unaotarajiwa kugharimu zaidi ya dola milioni 500 utaleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Kampuni ya Perseus nchini Tanzania, Lee Anne de Bruin ameishukuru serikali kwanamna inavyowapa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao huku akihaidi kuendelea kutekeleza makubaliano yote waliyoyasaini kwenye mikataba kwakufuata sheria,kanuni na taratibu za nchi.


Baadhi ya wananchi akiwemo Salome Selemani na Jonathan Mashaka walisema matarajio yao makubwa ni kupata ajira kupitia mradi huo ili kuinua maisha ya familia zao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI