Mahakama ya rufaa nchini Marekani imeamua kuwa ushuru mwingi uliotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump ni kinyume cha sheria, hivyo basi kutayarisha mpambano wa kisheria ambao unaweza kuathiri ajenda yake ya sera za kigeni.
Uamuzi huo unaathiri ushuru wa Trump, uliowekwa kwa nchi nyingi ulimwenguni, pamoja na ushuru mwingine uliowekwa kwa nchi za China, Mexico na Canada.
Katika uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya Marekani ya shirikisho ilikataa hoja ya Trump kwamba ushuru huo unaruhusiwa chini ya sheria ya dharura ya nguvu za kiuchumi, ikiziita "batili na kinyume cha sheria".
Uamuzi huo hautaanza kutekelezwa hadi tarehe 14 Oktoba ili kuwapa muda watawala kuitaka Mahakama ya Juu zaidi kushughulikia kesi hiyo.
Trump aliikosoa mahakama ya rufaa na uamuzi wake akisema: "Ikiwa itaruhusiwa kusimamishwa, uamuzi huu utaangamiza Marekani kihalisi."
"Leo Mahakama ya Rufaa ya Wanachama wa Juu ilisema kimakosa kwamba ushuru wetu unapaswa kuondolewa, lakini wanajua Marekani itashinda mwishowe," aliandika.
"Kama ushuru huu utasitishwa, litakuwa janga kubwa kwa nchi. Itatufanya kuwa dhaifu kifedha, na inabidi tuwe na nguvu."
0 Comments