Mahakama ya Afrika Kusini imeamua kuwa serikali ya Zambia inaweza kuurejesha nyumbani mwili wa rais wa zamani Edgar Lungu na kumfanyia mazishi ya kitaifa, licha ya upinzani wa familia yake.
Mahakama kuu ya Pretoria iliamua kuunga mkono taifa la Zambia, ambalo hapo awali lilikuwa limewasilisha ombi la kuzuia mipango ya familia ya kumzika kwa faragha nchini Afrika Kusini, ambako alifariki mwezi Juni.
Wakati huo, mawakili wa serikali ya Zambia walisema kuwa matakwa ya kibinafsi hayapaswi kupindua maslahi makubwa ya umma.
Mzozo huo unafuatia mzozo wa muda mrefu kati ya Lungu na mrithi wake, Rais Hakainde Hichilema, huku familia ya Lungu ikisema kuwa ameonyesha kuwa Hichilema hapaswi kuhudhuria mazishi yake.
Akitoa uamuzi huo, jaji Aubrey Ledwaba alisema serikali ya Zambia "ina haki ya kurejesha mwili wa marehemu rais" na akaamuru familia yake "kuusalimisha" mara moja kwa mamlaka.
Hakuna agizo lililotolewa juu ya gharama za maombi ya dharura.
Kufuatia kifo cha Lungu kutokana na ugonjwa ambao haujafahamika akiwa na umri wa miaka 68, familia ilitaka kusimamia taratibu za mazishi ikiwa ni pamoja na kurudisha mwili wake nyumbani, lakini mamlaka za Zambia zilitaka kudhibiti.
Serikali na familia yake baadaye walikubaliana kuwa angefanya mazishi ya serikali kabla ya mahusiano kuvunjika kutokana na mipango mahususi, na kusababisha familia hiyo kuchagua kufanyia mazishi nchini Afrika Kusini.
Lungu aliiongoza Zambia kuanzia 2015 hadi 2021 aliposhindwa uchaguzi na Hichilema kwa kura nyingi.
Baada ya kushindwa huko alijiondoa katika siasa lakini baadaye akarejea kwenye kinyang’anyiro hicho.
0 Comments