Header Ads Widget

RAIS DKT. SAMIA KUTWAA FOMU YA URAIS KWA TIKETI YA CCM AGOSTI 9


MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

 Zoezi hilo litafanyika kesho, Agosti 9, 2025, katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla amesema kuwa hatua hiyo inaashiria kuanza rasmi kwa msimu wa kampeni za uchaguzi kwa vyama vyote vya siasa nchini.

"Baada ya kuchukua fomu, Mheshimiwa Rais atarejea Makao Makuu ya CCM hapa Dodoma, ambapo atapokelewa rasmi na viongozi pamoja na wanachama wa chama chetu, na kupata fursa ya kuwasalimia wananchi," amesema CPA Makalla.

Ameongeza kuwa, Dkt. Samia anagombea kwa awamu ya pili ya uongozi wake kwa mujibu wa Katiba, baada ya kumaliza kipindi cha kwanza cha miaka mitano, ambacho kitaisha rasmi mwaka huu.

Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, ambapo vyama mbalimbali vya siasa vitashiriki kikatiba kuwani nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI