Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba vijijini mkoani Kagera kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Jason Rweikiza ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 6,465 akifuatiwa na Faris Buruhan aliyepata Kura 4619.
Akitangaza Matokeo hayo, Katibu wa CCM wilaya ya Bukoba vijijini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Jesca Ndyamukama amesema kuwa kura zilizopigwa ni 11,682, kura halali 11,582 na zilizoharibika ni kura 100
Katibu huyo amewatangaza Wagombea wengine ambao ni Fahami Mastawili ambaye amepata kura 239,Asted amepata kura 124,Edmund Rutaraka kura 89 na Philibart Bagenda kura 44.
0 Comments