Header Ads Widget

IDADI YA WATOTO WANAOOKOLEWA MITAANI YATISHA

Na Mwandishi Wetu

WATOTO zaidi ya 600 wameokolewa kutoka mitaana na baadaye kunganishwa na familia zao walikokuwa wanazurula na wengine kujihusisha na tabia hatarishi.

Idadi hiyo ni miongoni mwa watoto 7000 waliokusanywa kutoka mitaani na baadaye kuwekwa kwenye vituo wakiwa kwenye uangalizi maalum.

Hayo yamesemwa na Meneja Miradi wa Shirika la SOS Villages Tanzania, Nelson Mmari wakati wa warsha ya kutathmini miradi ya watoto wa mitaani inayotekelezwa katika nchi mbalimbali za Afrika.

Mmari amesema idadi hiyo ya watoto waliorudishwa kweye familia zao inaonyesha kuwa hatua ya kumuunganisha mtoto na familia yake ni ngumu, inahitaji muda, weledi, utulivu ili kuhakikisa kwamba jambo hilo linakuwa sehemu ya jamii.

“Ni jukumu letu waandishi wa habari, kujengea jamii uelewa, waone kuwapo watoto wa mitaani ni kushindwa kwetu sote kama jamii, kama watanzania. Niwaombe tuunganishe nguvu ya pamoja yakiwamo mashirika na watu binafsi walio tayari kushirikiana na SOS Children Villages tufanyekazi ya kuwatoa hao watoto mitaani.

Aidha, katika kuendelea kuainisha na kuwakusanya watoto wa mitaani, meneja huyo amesema SOS kwa kushirikiana na wadau wengine wameanzisha dawati kwenye Kituo cha mabasi cha Magufuli kilichopo Mbezi kwa ajili ya kuwachukua watoto wanaoingia Dar es Salaam kila siku kutoka mikoani.

Anasema zaidi ya watoto watano hadi 20 wanaingia jijini Dar es Salaam kila siku.

“Hao ni wanaokuja na mabasi pekee, lakini kuna wanaokuja kwa malori na treni, hivyo idadi ya watoto wanaiongia kila siku kwenye jiji hili ni kubwa,”amesema. Mmari.

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Doroth Gwajima ameitaka jamii kubeba kwa uzito matukio ya watoto kutoweka au kutoroka kwenye maeneo yao.

Sambamba na hilo amewataka watanzania kuripoti matukio yanayohusiana na changamoto za kijamii ili ziweze kupatiwa ufumbuzi badala ya kuziacha zikiendelea kujikita na kusababisha matatizo makubwa zaidi.

“Tuache kuthamini mifugo kuliko binadamu, katika jamii zetu, ng’ombe, mbuzi, kondoo akipotea watu hawalali wanajikusanya kwenda kutafuta mfugo huo, lakini mtoto akipotea au kutoroka hakuna anayejali. Niwaombe watanzania tubadilike, turipoti matukio haya kwa uzito unaostahili ili ufumbuzi upatikane.”amesema Waziri Gwajima.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI