Mgombea Ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi Bwana Adonis Bitegeko ni Mgombea pekee katika Jimbo hilo baada ya Chama Cha Ukombozi wa Umma kushindwa kurejesha fomu .
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muleba Kaskazini na Kusini Bwana Yona Charugamba wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa wilaya ya Muleba ina majimbo mawili ya Uchaguzi ambayo ni Muleba Kaskazini na Muleba Kusini ambapo Muleba Kusini ina kata 25 na Kaskazini ina kata 18
Amesema kuwa katika Jimbo la Muleba Kaskazini wagombea waliochukua fomu ni wawili ambao ni Bwana Adonis Bitegeko kutoka chama cha Mapinduzi na Eradius Kaitila ambapo mpaka wakati wa kufunga zoezi la Uchukuaji wa fomu alirejesha Bwana Adonis Bitegeko pekeee
Bwana Charugaba amesema kuwa Adonis Bitegeko ametimiza vigezo vyote vinavyotakiwa kujazwa kwenye fomu hivyo Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi imemteua kuwa Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini .
Ameongeza kuwa Vyama vingine havikujitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Muleba Kaskazini isipokuwa Chama cha Mapinduzi(CCM) pamoja na Chama Cha Ukombozi wa Umma ( CHAUMA) pekee ndo vilivyojitokeza katika zoezi hilo .
Kwa upande wa Jimbo la Muleba Kusini Kusini Jumla ya Vyama vitano vimejitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge ambavyo ni Chama cha Mapinduzi (CCM) , NCCR Mageuzi, TLP, ACT Wazalendo na CHAUMA ambapo wagombea kutoka vyama hivyo ni Bwana Oscar Kikoyo, Benezeti Josephat ,Abihudi Mbekomize ,Jonepo Rwakalela na Khamis Yusuph
0 Comments