Donald Trump amesema amesikitishwa na Putin lakini akasema bado hajakata tamaa na Vladimir Putin, katika mazungumzo ya kipekee ya simu na BBC.
Rais wa Marekani alishinikizwa iwapo anamuamini kiongozi huyo wa Urusi, na akajibu: "Sina imani na mtu yeyote."
Trump alikuwa akizungumza saa chache baada ya kutangaza mipango ya kutuma silaha kwa Ukraine na kuonya kuhusu ushuru mkali kwa Urusi ikiwa hakutakuwa na makubaliano ya kusitisha mapigano ndani ya siku 50.
Katika mahojiano marefu kutoka kwa Ofisi yake ya Oval, rais pia aliidhinisha Nato, baada ya mara moja kuielezea kama iliyopitwa na wakati, na kuthibitisha kuunga mkono kanuni ya ulinzi ya pamoja ya shirika hilo.
Rais Trump aliipigia simu BBC katika mazungumzo yaliyodumu kwa muda wa dakika 20, baada ya mazungumzo kuhusu mahojiano yanayoweza kuadhimisha mwaka mmoja tangu jaribio dhidi ya maisha yake lilipotokea katika mkutano wa kampeni huko Butler, Pennsylvania.
Alipoulizwa iwapo kunusurika kwenye jaribio la mauaji kumembadilisha, Trump alisema alipenda kulifikiria kidogo iwezekanavyo kuhusu hilo.
"Sipendi kufikiria ikiwa ilinibadilisha," Trump alisema. Kufikiria kulihusu, "inaweza kubadilisha maisha".
Baada tu ya kukutana na mkuu wa Nato Mark Rutte katika Ikulu ya White House, hata hivyo, rais alitumia sehemu kubwa ya mahojiano kuelezea kwa mapana kuhsuu kukatishwa tamaa kwake na kiongozi wa Urusi.
Trump alisema kuwa alifikiri kwamba makubaliano yalikuwa kwenye yamefikiwa na Urusi mara nne tofauti.
0 Comments