Header Ads Widget

TRUMP AAHIDI KUIPATIA SILAHA UKRAINE

 

Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumatatu kwamba Marekani itatuma silaha zaidi nchini Ukraine.

Wiki iliyopita , Pentagon ilitangaza kuwa inasimamisha usambazaji kwa Ukraine, na msemaji wa White House alielezea Jumatatu kwa nini ilifanya hivyo.

"Tutawatumia silaha zaidi. Tunahitaji kufanya hivyo. Tunahitaji waweze kujilinda. Wanapigwa sana hivi sasa. Wanapigwa sana. Itabidi tutume silaha zaidi, ndiyo, silaha za kujilinda zaidi. Lakini wanapigwa sana, tena sana. Watu wengi wanakufa katika fujo hii," Trump aliripoti.

Trump aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kutofurahishwa na tabia ya Putin.

Trump hakuingia kwa undani zaidi kuhusu vifaa hivi vinavyodaiwa kuwa vipya kwasababu kilikuwa ni kipindi kifupi cha maswali na majibu kuhusu mada mbalimbali kabla ya chakula cha jioni na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Wiki iliyopita, serikali ya Marekani ilitangaza kusitisha usafirishaji wa silaha kwa Ukraine, ikielezea wasiwasi kwamba hifadhi za Pentagon zimepunguzwa sana.

Vyombo vya habari vya Magharibi viliripoti kuwa Marekani imesitisha uwasilishaji wa aina fulani za makombora ya kutungulia ndege na zana zingine zinazoongozwa kwa usahihi kwa Ukraine.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI