Header Ads Widget

SIMON SIRRO ATUMA UJUMBE MAJAMBAZI WALIOTEKA KIGOMA

 


Na Fadhili Abdallah Kigoma

Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amesema kuwa amekasirishwa na kitendo cha uhalifu cha kuteka magari kilichotokea wilayani Kibondo mwishoni mwa wiki ilipita na kwamba hatua madhubuti zimechukuliwa kukabiliana na wale wote waliohusika na tukio tukio.

Kamanda Sirro alisema hayo katika kikao na watumishi wa manispaa ya Kigoma ikiwa ni muendelezo wa ziara yake kutembelea wilaya kukagua miradi na kuzungumza na watumishi ambaapo alisema kuwa kama wahalifu wamembip basi yeye anawapigia.

Alisema kuwa taarifa zinaonyesha kuwa viyendo vya utekaji vilikuwa vimekomeshwa lakini sasa wahalifu wameonyesha kwamba bado wapo hivyo kupitia vikosi vya ulinzi na usalama vitafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha waliofanya uhalifu katika tukio la Kibondo wanakamatwa.



Katika mkutano huo na watumishi Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa kwa sasa hana maneno mengi baada ya tukio hilo lakini majibu yataonekana huku akiwaonya watu wote kutojihusisha na wahalifu na vitendo vya kihalifu kwani sheria kali dhidi yao zitachukuliwa.

Julai 11 mwaka watu wanaoaminika kuwa majambazi waliteka basi la abiria la kampuni ya Adventure kilometa mbili kutoka kambi ya wakimbizi wa Burundi ya Nduta wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma ambapo mali mbalimbali za abiria ziliporwa kwenye tukio hilo.

Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Filemon Makungu alisema kuwa taarifa walizokusanya kutoka kwa abiria waliokuwa kwenye gari zilizotekwa likiwemo basi la abiria na gari ndogo aina ya Toyota Kluger alisema kuwa majambazi walipora fedha taslim kiasi cha shilingi milioni 3.5, komputa mpakato moja na  simu tatu za mkononi.





 





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI