Header Ads Widget

MKUTANO WA PILI WA MABARAZA HURU YA HABARI AFRIKA FURSA KWA NCAA KUTANGAZA VIVUTIO VYAKE.

 


Na,Jusline Marco;Arusha

Katika Mkutano wa pili wa Mabaraza huru ya Habari Afrika unapendelea jijini Arusha, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) inatumia fursa ya mkutano huo kunadi vivutio vya utalii vilivyopo katika eneo la Hifadhi Ngorongoro ili kuendelea kuwavutia wageni wengi zaidi.

Afisa Utalii Mkuu NCAA Peter Makutian ameeleza kuwa ushiriki wa NCAA katika mkutano huo unalenga kuwafikia wajumbe wa mkutano huo na kuwaelezea vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro ambayo ni kivutio Bora cha Utalii Afrika kwa mwaka  2023 na mwaka 2025.

"Kama mnavyojua Ngorongoro ni kivutio Bora cha utalii Afrika hivyo wageni wanahamasika na kuwa na shauku ya kujua vivutio vilivyopo,  fursa za uwekezaji na shughuli za utalii, kwa siku zote za mkutano huu tutahakikisha tunawafikia na kuendelea kutangaza eneo letu" alisema  Makutian.


Mkutano huo ulioanza Julai 14 mwaka huu Jijini Arusha utahitimishwa Julai 17, 2025 umewakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Habari kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika ambapo washiriki zaidi ya 200 wanahudhuria mkutano huo.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni;  "Kuendeleza kanuni za vyombo vya habari na mawasiliano kwa ubora wa uandishi wa habari barani Afrika".



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI