Header Ads Widget

RAIS SAMIA KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA DODOMA




Na Hamida Ramadhan, Matukio Madia App Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kumbukizi ya Mashujaa yatakayofanyika Julai 25, mwaka huu, katika Uwanja wa Mashujaa, Mtumba jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, alisema maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika na yataambatana na gwaride rasmi la heshima kwa vikosi vya ulinzi na usalama.


“Tukio hili ni muhimu kwa taifa letu Tunawakumbuka mashujaa wote waliopoteza maisha wakati wa vita mbalimbali pamoja na wale waliostaafu baada ya kulitumikia taifa kwa uaminifu na ujasiri,” alisema Dkt. Biteko.

Aidha, alibainisha kuwa kama sehemu ya kumbukizi hizo, mwenge wa mashujaa utawashwa Julai 24, siku moja kabla ya maadhimisho, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa kipindi cha maombolezo ya kitaifa kwa ajili ya kuwaenzi mashujaa hao.

 “Mwenge huo wa kumbukizi utawashwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, kwa niaba ya Mhe. Rais, na utaendelea kuwaka hadi saa sita usiku wa Julai 25, 2025,” aliongeza.

Siku ya Mashujaa uadhimishwa kila  ifikapo Julai 25 kama heshima kwa Watanzania waliotoa mchango mkubwa katika kulitumikia taifa, hasa katika nyakati za vita, migogoro au katika kulinda amani na uhuru wa nchi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI