Header Ads Widget

PATO LA TAIFA KUWA DOLA TRIL.1 KUFIKIA 2050

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

Kufikia 2050 Tanzania itakuwa imekuza Pato la Taifa kutoka $88.4bn hadi $1Trl.

Moja ya shabaha za Dira 2050 ni kuchochea ukuaji wa Pato la Taifa kutoka $88.4bn ya sasa mpaka$1 Trilioni ifikapo mwaka 2050 miaka 25 baadae.

Thamani ya Pato la Taifa kwa mwaka 2000 ilikuwa ni $13.37bn sawa na TZS 35 Trilioni, leo miaka 25 baadae limefikia wastani wa $88.4bn sawa na TZS 230 Trilioni.

Idadi ya watu tangu wakati huo imeongezeka kwa wastani wa kati ya 2.7% hadi 3.2%, kwa wastani idadi hii kati ya mwaka 2000 hadi mwaka 2024 imeongezeka kwa mara mbili, Ikiwa wastani wa ukuaji wa uchumi kwa miaka 25 wastani wake ni 6% maana yake ukuaji pia utaongezeka pia mara mbili na kufikia ukuaji wa kati ya 10-12 (demographic devident).

Ifikapo mwaka 2050 inatarajiwa idadi ya watu pia itafikia makisio ya watu 120M kutoka watu 61M wa sasa kutokana na historia ya nyuma ya idadi ya watu kuongezeka mara mbili kila baada ya miaka ishirini na tano(25).

Kwa mantiki hiyo, ifikapo mwaka 2050 Tanzania kuwa na pato la taifa lenye thamani ya $1trilioni au TZS 2,600 Trilioni na wastani wa pato la mtu mmoja lenye thamani ya $7,000 sawa na TZS18.2milioni kwa mwaka au TZS1,520,000 kwa mwezi, sawa na TZS50,556 kwa siku, kutoka $1,277 kwa mwaka (sawa na TZS3,320 kwa mwaka TZS276,688 kwa mwezi au TZS9,233 kwa siku) za sasa.

Ifikapo 2050, huduma ya maji safi na salama itawafikia Watanzania wote. Dira ya awali (2000-2025) ililenga kuwa watu waishio vijijini wanapata maji safi kutoka 50% mwaka 2000 hadi kufikia 85% mwaka 2025 na watu waishio mjini wanapata maji kutoka 50% mwaka 2000 mpaka 95% mwaka 2025.

Mpaka Desemba 2022, 77% ya watu waishio vijijini walipata huduma ya maji safi na salama na 88% wa mjini walikuwa wamefikiwa na huduma ya maji. Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu upatikanaji wa maji mijini umeongezeka kutoka asilimia 84% hadi 91.6%, na vijijini kutoka 70.1% hadi 85%.

Wakati anaingia madarakani serikali ilikuwa imefikisha maji kwa vijiji 5,258, mpaka kufikia mwaka 2025 amefikisha vijiji 10,779 sawa na ongezeko la vijiji 5,521.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI