Header Ads Widget

MSIGWA, MSAMBATAVANGU WAPETA MCHUJO WA CCM UBUNGE IRINGA MJINI



Mbunge wa sasa wa Jimbo la Iringa Mjini Jesca Msambatavangu na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya  CHADEMA, Mchungaji Peter Simon Msigwa, wametajwa miongoni mwa wagombea waliofanikiwa kupita katika mchujo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Majina ya wagombea waliopitishwa yametangazwa leo Julai 29, 2025, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, katika mkutano uliofanyika makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma.

Mbali na Msambatavangu na Msigwa, wagombea wengine waliopitishwa katika mchujo wa Jimbo la Iringa Mjini ni Moses Ambindwile, Fadhili Ngajilo, Edward Chengula na Islam Huwel.









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI