Na Matukio Daima Media
Msanii maarufu wa kizazi kipya, Faustine Mfinanga(Nandy), ameomba Watanzania kuitangaza kwenye shughuli zao nembo ya 'Made in Tanzania' nje na ndani ya Tanzania.
Nandy ametoa kauli hiyo alipotembelea Banda la Made in Tanzania, kwenye maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF) katika viwanja vya sabasaba, Temeke.
"Nimevutiwa sana na namna nembo hii inavyotambulisha bidhaa zetu huko duniani. Sasa ni wakati na sisi tuitumie kuitangaza kupitia bidhaa zetu na shughuli zetu na mimi nitakuwa miongoni mwa watakaoitumia sana kwenye shughuli zangu za muziki na bidhaa ninazouza.
"Pia, nitakuwa Balozi wake, ninaomba Watanzania wenzangu tuunge mkono hili na kila mmoja kwa nafasi yake aitangaze nembo yetu."
Nembo ya Made in Tanzania inasimamiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE), na inalenga kuimarisha utambulisho wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mwisho.
0 Comments