Morogoro
Zoezi la kura za maoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupata Mbunge wa Viti Maalum limekamilika, ambapo Lucy Kombani, mtoto wa Waziri wa zamani aliyehudumu katika Wizara mbalimbali Marehemu Celina Kombani, ameibuka mshindi kwa kupata kura 1314.
Lucy kombaniKatika uchaguzi huo uliosimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima, Aliyefuata ni Mkurugenzi wa zamani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Bi Sheila Lukuba aliyepata kura 597.
Sheila lukuba
Wagombea wengine walioshiriki na kura walizopata kwenye mabano ni Josephine Kapoma (454), Jane Mihanji (339), Aliyah Awadhi Omary (236), Amina Karuma (153), Hajira Mwikoki (90), Dkt Kulwa Kangeta (75) na Rachel Mashishanga (35).
0 Comments