Header Ads Widget

MAREKANI YASEMA ‘HATUA ZA KIPEKEE’ ZIMEAFIKIWA KUMALIZA GHASIA BAADA YA ISRAEL KUIPIGA DAMASCUS

Jeshi la Israel limeishambulia wizara ya ulinzi ya Syria mjini Damascus na vikosi vya serikali kusini mwa Syria siku ya Jumatano, huku mapigano makali ya kimadhehebu katika mkoa wa Druze wa Suweida yakiendelea kwa siku ya nne.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema vikosi vyake "vinafanya kazi kuwaokoa ndugu zetu wa Druze na kuyaangamiza magenge ya utawala huo". Wizara ya mambo ya nje ya Syria iliishutumu Israel kwa "uchokozi wa kiuhaini".

Zaidi ya watu 300 wanaripotiwa kuuawa huko Suweida tangu Jumapili, wakati mapigano kati ya wanamgambo wa Druze na makabila ya Bedouin yalipozuka.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio alisema "ana wasiwasi sana" na ghasia kusini mwa nchi hiyo lakini anaamini kwamba zitaisha baada ya saa chache.

"Tumekubaliana juu ya hatua maalum ambazo zitamaliza hali hii ya kutatanisha na ya kutisha usiku wa leo," aliandika kwenye X Jumatano jioni.

Wizara ya mambo ya nje ya Syria ilisema nchi hiyo "inakaribisha juhudi zinazofanywa na Marekani na pande za Uarabuni" za "kusuluhisha mgogoro uliopo" kwa amani.

Israel bado haijatoa maoni yoyote kuhusu mpango wa kusitisha mapigano.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI