Header Ads Widget

KIGOMA YANG'ARA KWENYE CHIKICHI: UZALISHAJI WAONGEZEKA KWA 40%

 


Na Hamida Ramadhan, MatukuoDaima Media ,Dodoma 

MKOA wa Kigoma umeendelea kufanya vizuri katika sekta ya kilimo, hususan katika uzalishaji wa zao la chikichi, ambapo uzalishaji umeongezeka kutoka tani 25,000 mwaka 2020/2021 hadi tani 35,000 mwaka 2024/2025, sawa na ongezeko la asilimia 40.


Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amesema katika juhudi za kuongeza tija kwenye zao hilo, uzalishaji wa mbegu bora za chikichi aina ya TENERA umeimarika kutoka mbegu milioni 1.6 mwaka 2020/2021 hadi milioni 2.9 mwaka 2024/2025, sawa na ongezeko la asilimia 85.4.



Mkuu wa Mkoa Sirro ameeleza Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, serikali imenunua pikipiki 153, vipima udongo 5, na magari 2 kwa ajili ya maafisa ugani na wakaguzi wa kilimo, ili kuongeza ufanisi na kuwafikia wakulima kwa haraka zaidi.


"Katika kipindi hicho hicho, jumla ya maafisa ugani 93 wameajiriwa mkoani Kigoma, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali ya awamu ya sita kuboresha huduma za ugani," Amesema 


Na kuongeza " Maafisa wengine saba wamepangwa mkoani humo kupitia programu ya Jenga Kesho Iliyobora (BBT)," Amesema.


Ameeleza Kupitia mfumo wa ruzuku ya pembejeo, matumizi ya mbolea yameongezeka kutoka tani 21,780 mwaka 2020/2021 hadi tani 40,296 mwaka 2024/2025, ongezeko la asilimia 85, hatua inayochangia kuongeza uzalishaji kwa wakulima wa mazao mbalimbali.


Amesema Katika hatua nyingine, idadi ya vyama vya ushirika imeongezeka kutoka kimoja mwaka 2020/2021 hadi vinane mwaka 2024/2025, sawa na ongezeko la asilimia 700.


" Jambo hilo limeongeza ushirikishwaji wa wakulima katika masuala ya masoko, mikopo na usimamizi wa rasilimali, " Amesema Mkuu wa Mkoa huyo. 


Miundombinu kwa Watumishi Yaboreshwa


Serikali pia imefanikiwa kujenga nyumba 4 za watumishi wa sekta ya kilimo katika maeneo ya vijijini, kwa lengo la kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza uwepo wa wataalamu. 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI