Header Ads Widget

KAMISHNA BADRU APONGEZA JITIHADA ZINAZOFANYWA ZA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII NCHINI.

 


Na,Jusline Marco ;Dar es Salaam

Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Abdul-Razaq Badru amesema ushiriki wa Ngorongoro katika maonesho mbalimbali ni ili kujitangaza , ambapo mamlaka hiyo inaendelea kufanya jitihada za kuboresha miundombinu ya utalii kama barabara, huduma za malipo, malazi kwa wageni na huduma za usafiri.

Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya banda la NCAA wakati alipotembelea kwenye maoneshoo ya 49 ya biashara ya Kimataifa Sabasaba, Kamishna Badru amezipongeza taasisi hiyo kwa kushinda tuzo nyingi zilizotolewa na mtandao wa World Travel Awards (WTA) Juni 28 mwaka huu na kupongeza kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.


“Tumejipanga mwaka huu wa fedha kuhakikisha kuwa barabara zetu zinaboreshwa na kupitika muda wote, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali jitihada zinaendelea kuongeza miundombinu ya malazi na huduma za usafiri ili kukidhi ongezeko la wageni wanaotembelea vivutio vyetu kila mwaka,”alisema Kamishna Badru.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inashiriki maonesho hayo ili kuendelea kutangaza vivutio vya utalii kwa watembeleaji wa eneo hilo. 

Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro mwaka huu 2025 limetangazwa na mtandao wa world Travel Awards  ( WTA) kuwa  kivutio bora cha utalii baranı Afrika ikiwa ni mara ya pili baada ya kushinda tuzo hiyo mwaka 2023.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI