Donald Trump anaugua ugonjwa sugu wa mshipa, Ikulu ya Marekani ilitangaza siku ya Alhamisi, baada ya siku kadhaa za uvumi kuhusu picha zinazoonyesha michubuko kwenye mkono wa rais huyo wa Marekani.
Baada ya hivi karibuni kupata uvimbe kwenye miguu yake, Trump alifanyiwa "uchunguzi wa kina" ikiwa ni pamoja na upimaji wa mishipa ya damu, kulingana na Katibu anayehusika na Vyombo vya Habari wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt.
Leavitt alisema hali ya mkono wa Trump ulioonekana kuvimba ilitokana na "uharibifu wa tishu kutokana na kusalimiana kwa mara kwa mara" wakati akitumia dawa ya aspirini, ambayo alisema ni "sehemu ya utaratibu wa kawaida wa kudhibiti moyo na mishipa".
Trump, mwenye umri wa miaka 79, amekuwa akisifu afya yake mara kwa mara na aliwahi kujieleza kuwa "rais mwenye afya njema zaidi kuwahi kuishi".
Ugonjwa wa mshipa wa rais uliogunduliwa hivi majuzi unaitwa -chronic venous insufficiency , ambao hutokea wakati mishipa ya miguu inaposhindwa kusukuma damu kwenda kwenye moyo, na hivyo kusababisha kujikusanya mishipa ya damu katika sehemu za chini za miguu, ambayo inaweza kusababisha kuvimba.
0 Comments