Header Ads Widget

FC BARCELONA YAKUBALI KUITANGAZA DRC KWA DOLA MILIONI 46

 

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imekubali kulipa klabu ya soka ya Uhispania FC Barcelona dola milioni 46 ili kuitangaza nchi hiyo kwa nia ya kuimarisha utalii wake, kwa mujibu wa makubaliano na Reuters.

Makubaliano hayo ya tarehe 29 Juni (6) yanaeleza kuwa nembo inayoonyesha nchi hiyo kama "moyo wa Afrika" itaonekana nyuma ya vifaa vya mazoezi vya timu za Barcelona za wanaume na wanawake.

'Nembo' hiyo pia itaonekana kwenye matangazo ya klabu, kwenye jarida lake na katika ripoti ya kila mwaka ya klabu, kwa mujibu wa makubaliano.

DR Congo italipa kati ya dola milioni 11 na milioni 13 kwa mwaka katika kipindi cha miaka minne cha mkataba huu.

Vilabu vya Ufaransa AS Monaco na vilabu vya Italia AC Milan pia vilitangaza mwezi uliopita, bila kufichua ni kiasi gani walilipwa, katika mikataba waliyosaini na DRC.

Siku ya Jumatano, Moïse Katumbi, kiongozi wa chama kinachoipinga serikali cha Ensemble Pour La Republique, alimuandikia barua Rais Félix Tshisekedi, akisema kwamba mikataba hiyo ni "tusi kwa mateso ya watu wa Congo."

Katika barua yake, Katumbi ambaye kwa sasa anaimiliki TP Mazembe alisema: "Wanatumia mamilioni ya dola kusaidia klabu tajiri za Ulaya huku wameshindwa kutoa dola 600,000 ili kumaliza msimu wetu wa soka. Je, ni muhimu kukukumbusha kuwa msimu wetu ulisimamia katikati kwa kukosa fedha?..."

Didier Budimbu, waziri wa michezo wa DR Congo, aliambia Reuters kwamba kandarasi na AS Monaco ina thamani ya dola milioni 1.8 kwa mwaka. Hakusema AC Milan italipwa kiasi gani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI