Header Ads Widget

BALOZI KOMBO AMEENDELEA KUFANYA MIKUTANO NA VIONGOZI NA WADAU MBALIMBALI KUIMARISHA UHUSIANO BAINA TANZANIA NA MAREKANI


Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameendelea kufanya mikutano na Viongozi na wadau mbalimbali muhimu katika kukuza na kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Marekani. Miongoni mwa Viongozi hao ni Mhe. Dkt. Ronny L. Jackson, Mwanachama wa Kamati Ndogo ya Afrika ya Bunge la Wawakilishi la Marekani. 

Pamoja na masuala mengine, Mhe. Dkt. Jackson alimweleza Mhe. Waziri kuwa amewahi kufika Tanzania na anavutiwa na uzuri wa nchi, na pia  anafikiria kuongoza Ujumbe utakaojumuisha Wabunge wengine kuitembelea tena Tanzania mwaka 2026 kufuatia mwaliko kutoka kwa Mhe. Waziri.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI