Header Ads Widget

HALIMA YAHAYA MPINGE ‘DAVINA’ AOMBA KURA ZA USHINDI – "NASHUKURU CHAMA KUNITEUA"

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

IRINGA

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na msanii maarufu wa filamu nchini, Halima Yahaya Mpinge, anayefahamika zaidi kwa jina la kisanii Davina, ametoa shukrani zake kwa chama hicho kwa kumteua kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum Taifa kundi la NGOs.

Akizungumza na Matukio Daima Media baada ya uteuzi huo, Davina alisema anashukuru kwa kuaminiwa na chama Taifa na kuteuliwa kugombea.


"Nashukuru sana chama changu kipenzi CCM kwa kuniamini na kuniteua kuwa mgombea wa nafasi hii muhimu. Naomba kura zenu ndugu zangu, hasa wajumbe, ili tuweze kushinda na kuendelea kuwahudumia wananchi."

Ameongeza kuwa huu si mara yake ya kwanza kujaribu nafasi hiyo, kwani aligombea pia mwaka 2020 lakini hakufanikiwa kutokana na kura kutotosha.

"Nilijaribu mwaka 2020 lakini kura hazikutosha, leo nimerudi tena kwa nguvu mpya na ari mpya," alisema Davina.

Kwa sasa, Davina ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa na Maadili ya Wilaya ya Iringa Vijijini pamoja na kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Iringa.

Amewahakikishia wajumbe kuwa atakuwa sauti ya wanawake na vijana bungeni endapo atapata nafasi hiyo, huku akisisitiza kuwa nia yake ni kuendeleza juhudi za maendeleo kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Hivyo amewaomba wajumbe wa mkutano mkuu maalum utakaofanyika jumamosi kumpa kura za kishindo ili kwenda kuwatumikia .


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI