NA ZUHURA ZUKHERI MATUKIO DAIMA MEDIA ,IRINGA
KATIBU mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma Salum Mwalimu amesema Chama hicho hawana mpango wa kususia uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 kwa sababu ya mihemko ya baadhi ya wanasiasa wa upinzani wenye mslahi binafsi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara chini ya Operesheni Chaumma For Change (C4C) uliofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa Manispaa ya Iringa leo Mwalimu amesema chauma haitaingia katika mkumbo wakususia uchaguzi kwa kuwa hakuna mabadiliko yoyote yanayoweza kufanyika kwa kususia uchaguzi.
Amesema kuwa kuna madhara makubwa ambayo yanaweza kujitokeza endapo kama watu wataungana na baadhi ya vyama vya upinzani katika kususia uchaguzi, kwani Ccm itashinda maeneo yote ya uongozi hivyo atakosekana muwakilishi atakayeenda kupigania mageuzi ndani ya serikali jambo ambalo litaendela kukosa uvumbuzi katika kipindi kingine tena cha uchaguzi.
Akitolea mfano wa wanasiasa wakubwa katibu mkuu huyo wa CHAUMA Salim Mwalimu amesema kuwa Leyla Odinga ni mwanasiasa mkubwa na amekutana mambo magumu katika siasa lakini hawakuwahi kususia uchaguzi kama tunavyoshawishiwa na baadhi ya watu wachache wenye ubinafsi.
“Ndugu zangu wana Iringa nani asiyemjua mwanasiasa mkubwa Layla Odinga amekutana na hekaheka ngumu za kisiasa lakini hakuwahi kususia uchaguzi, sio yeye wapo wanasiasa wengi wakubwa nao wamekuwa na wakati mgumu katika siasa hatujawahi kusikia wanasusia uchaguzi vipi sisi tushawishiwe nah awa watu wenye maslahi bianafsi tukasuse uchaguzi sisi CHAUMA tunasema hatususi hatuwezi kuwapa wepesi CCM kuingia katika Madaraka hilo Hapana”alisema Mwalimu
Alisema kitendo cha kususia uchaguzi ni ishara ya woga na hofu ya kuingia katika katika mapambano jambo ambalo CHAUMA wamelikataa huku akijinadi kuweka wagombea wanaokubalika katika kata na majimbo yote ya mkoa wa Iringa ili kuiondoa CCM madarakani.
Alisema kuwa amekuwa katika chama kikuu cha upinzani kwa muda lakini hajawahi kuwa na hofu ya kuiondosha CCM madarakani na wapo CHAUMA kuendeleza mapambano ya kuiondoa CCM madarakani na mwaka huu lazima iondoke madarakani.
Makamu mwenyekiti wa CHAUMA Tanzania bara Devota Minja amesema endapo wananchi watashawishika kususia uchaguzi watakuwa wameipitisha CCM kiurahisi kushinda kata na majimbo yote na kushindwa kufanya mabadiliko wanayo yahitaji.
Amesema kususia uchaguzi sio dawa ya kupata mageuzi bali wanachotakiwa ni kchagua madiwani, wabunge na Rais kutoka CHAUMA ambao watakwenda kuisukuma serikali katika kufanya mabadiliko ya kweli.
“Wanairinga niwaambie mkithubutu kususia uchaguzi mtajumiza wenyewe maana CCM watakomba viti vyote vya udiwani, watakomba viti vyote vya ubunge na pia hata uraisi wataubeba hayo mageuzi wanayolilia hao viongozi wenye ubinafsi watayapata wapi wakati hamtapeleka muwakilishi? “alihoji Devota Minja
Fatuma Musi ni mkazi wa Manispaa ya Iringa anasema CHAUMA wamekomaa kisiasa kwani sera walizozitoa sio za kususia uchaguzi bali wamewaelimisha wananchi Kwenda kupiga kura na kuitoa CCM madarakani.
Fatuma alisema hakuna mageuzi yoyote ya kisheria ambayo yanaweza kupatikana kama viongozi wa siasa za upinzani wamekuwa wakihamasisha wanananchi wasusie uchaguzi maana yake wanataka kuipa nafasi CCM ya kupita bila kuwa na ugumu.
Alisema Sera zilizotolewa na CHAUMMA zimekuwa ni za kistaarabu kwani hazina uchochezi wala maeneo yenyekuashiria uvunjifu wa amani jambo ambalo kama vyama vyote vya upinzani vingefanya hivyo kusikuwa na mihemko tunayoishuhudia kwa baadhi ya wanasiasa.
0 Comments