Baadhi ya wawakilishi wa vyuo vikuu wakiwasili nchini kwa maonyesho ya elimu yanayotarajiwa kufanyika Jumanne wiki ijayo
Na Matukio Daima Media
WAKALA wa Elimu Nje ya nchi Global Education Link inatarajia kuwakutanisha wanafunzi wa Tanzania na vyuo vikuu zaidi ya 20 kutoka nchi mbalimbali duniani katika maonyesho jijini Dar es Salaam ambapo wanafunzi watapata fursa ya kujua fursa za kusomea kozi mbalimbali kwenye vyuo hivyo.
Global Education Link imesema wanafunzi watakaotaka kusoma nje ya nchi watapata udahili wa papo hapo.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel, wakati akizungumza kuhusu maonyesho hayo.
Alisema kwenye maonyesho hayo yatakayofanyika siku ya Jumanne Julai 22 kutakuwa na vyuo vikuu kutoka mataifa mbalimbali vikiwemo kutoka nchi za Cyprus, India China Malaysia, Uingereza, Canada, Marekani, Australia, Uturuki , Mauritius na Dubai
Alisema baadhi ya vyuo vikuu vitakavyoshiriki kwenye maonyesho hayo vitatoa ufadhili wa kuanzia asilimia 20 hadi 80 wakati vingine vitatoa ufadhili wa moja kwa moja.
Mollel alisema kwa wanafunzi wanaotaka kusomea Shahada za Uzamili na Uzamivu hasa kwenye masomo ya uhandisi watapewa ufadhili kwa asilimia 100.
“Ndani ya maonyesho hayo vyuo vikuu kutoka Cyprus, India China Malaysia, Uingereza,Canada Marekani, Australia, Uturuki , Mauritius Dubai vyuo vitatoa udahili wa papo kwa papo kwa hiyo wanafunzi waliomalisa sekondari wachangamkie fursa hii,” alisema .
Aliwahakikishia wazazi kuwa kuna uhakika wa kupata udahili ilimradi mwanafunzi awe amefaulu na kwamba watapata vyuo vikuu bora ambavyo vinatambulika na nchi zao na mamlaka za ithibaki ndani ya Tanzania
“Wanafunzi watakaokuja watapata vyuo vya kimataifa kwenye kozi mbalimbali na gharama ni zile zile kama za vyuo vya ndani ya nchi,” alisema
“Tumezingatia vyuo vikuu ambavyo vinamalezi na usalama kwa wanafunzi na ambavyo vinauwezo wa kutoa nyaraka zitakazomwezesha mwafunzi kwenda chuo kikuu kwa wakati, vyuo vikuu vyenye malazi na ambavyo vimekidhi vigezo vya ithibati na ubora wa kozi wanazotoa,” alisema
“Njia za kushiriki kwenye maonyesho ziko tatu, kwa anayetamani kuja Serena hotel kuanzia asubuhi na ushiriki wa kufanya miadi kwa kupiga simu kutaka kujua chuo unachotaka kusoma na watu wa GEL watapokea simu na kukupa taarifa unazotaka,” alisema
“Unaweza ukaingia kwenye tovuti ya Global Education Link ukapata taarifa zote ukajaza taarifa zako na ukapata udahili wa haraka sana,” alisema
Alisema urithi wa mtoto ni elimu na GEL imeona umuhimu wa kutoa mchango wake kwa kuwaletea vyuo vikuu vya nje na kuwapa udahili wa hapo hapo wanafunzi wanaohitaji kusoma nje ya nchi.
0 Comments