Polisi nchini Brazil wamevamia nyumba ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Jair Bolsonaro na kumwamuru kuvaa kifaa cha ufuatiliaji mguuni huku wakimzuia kutumia mitandao ya kijamii.
Hatua hiyo ni agizo kutoka Mahakama Kuu ya Brazil kutokana na hofu kuwa Bolsonaro anaweza kukimbia nchi wakati kesi yake ikiendelea ya kupanga njama ya kupindua matokeo ya urais wa mwaka 2022 ili aendelee kubaki madarakani.
0 Comments