Header Ads Widget

AJALI YAUWA WATU WATATU KILOLO..

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

Watu watatu wamefariki dunia na wengine 6 wamejeruhiwa katika ajali ya Basi huku chanzo kikielezwa kuwa ni  uzembe wa dereva wa basi kushindwa kulimudu gari lake na kugonga kwa nyuma gari lililokuwa limesimama mbele yake.

Akizungumza kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi alisema kuwa ajali hiyo imetokea Julay 18, 2025 saa 12 asubuhi kwenye kijiji cha Imalutwa Kata ya Lugalo, Tarafa ya Mazombe Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa katika barabara kuu ya Morogoro Iringa.

ACP Bukumbi ameeleza kuwa gari lenye namba za usajili T 562 EBK aina ya Fuso Mini Bus inayomilikiwa na Khatibu Kihwelo likiendeshwa na dereva Akhan Mpagile (45) mkazi wa Njombe ambaye amefariki kwenye ajali hiyo iligonga kwa nyuma gari lenye namba T857DVZ na Trela namba T460EAM aina ya Howo mali ya Glenrich Transportation Co Ltd lililokuwa likitokea Dar es salaam likiwa limebeba mzigo wa unga ambapo dereva wa Lori hilo alikimbia baada ya kutokea kwa ajali.

"Waliofariki ni dereva wa Minibus na wengine ni Alfred Mgaya mkazi wa Njombe ambaye ni utingo wa basi hilo na Feleschina Masigati (36) mkazi wa Imalutwa aliyekuwa abiria"alisema.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda raia na mali zao kwa kufanya operesheni mbalimbali za kupambana na uhalifu.

MWISHO.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI