Header Ads Widget

198 KATI YA 201 WALIOCHUKUA FOMU ZA UBUNGE CCM MORO WAREJESHA FOMU, WATATU WAINGIA MITINI


NA MATUKIO DAIMA MEDIA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Morogoro kimetoa taarifa ya kumaliziwka kwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba kuteuliwa na kugombea nafasi za Ubunge wa Majimbo na Viti Maalum, kwa kipindi kilichoanzia Juni 28 hadi Julai 2 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Morogoro, Bw.Zangina Shanang Zangina, jumla ya wanachama 201 walichukua fomu kugombea Ubunge wa Majimbo 11 ya mkoa huo, huku 198 kati yao wakirejesha fomu hizo. Majimbo ya Kilombero pekee yakishuhudia wagombea watatu kushindwa kurejesha fomu kutokana na sababu binafsi.

Kwa upande wa Jumuiya, wagombea wa Umoja wa Vijana wamekamilisha urejeshaji wa fomu 4 kati ya 5 zilizochukuliwa, Umoja wa Wanawake wote 31 wamerejesha fomu walizochukua, na kwa upande wa Wazazi wa CCM, wagombea wote wawili walirejesha fomu baada ya kuzijaza kikamilifu.

Mchakato unaofuata ni hatua ya vikao vya mchujo kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa, ambapo majina matatu kutoka kila kundi yatawasilishwa kwa ajili ya upigaji kura na hatimaye kupelekwa kwenye Mikutano Mikuu ya CCM na Jumuiya zake kwa ajili ya uteuzi wa mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI