Header Ads Widget

18 WAFARIKI NA NJAA GAZA NDANI YA SAA 24

 

Siku ya Jumapili Wiza ya Afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema imerekodi vifo 18 "kutokana na njaa" katika muda wa saa 24 zilizopita.

Siku ya Jumamosi wizara hiyo ilionya kwamba njaa kali inaongezeka huko Gaza na idadi ya watu wanaofika katika vituo vyake "wakiwa na uchovu mwingi inaongezeka."

"Tunaonya kwamba mamia ya watu ambao miili yao imechoka wako katika hatari ya kifo kutokana na njaa," ilisema.

Umoja wa Mataifa pia umesema raia huko Gaza wanakufa njaa na kutoa wito wa kuingizwa kwa haraka bidhaa muhimu.

Nje ya hospitali Shifa katika mji wa Gaza mwanamke mmoja aliiambia BBC Arabic kwamba "watu wanakufa".

"Watoto wanakufa kwa njaa kwa sababu hawana chakula. Watu wanaishi kwa maji na chumvi... maji na chumvi tu," alisema.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika taarifa iliyotumwa kwenye X, WFP ilisema "utapiamlo unaongezeka huku wanawake na watoto 90,000 wakihitaji matibabu ya haraka". "Takriban mtu mmoja kati ya watatu hawali kwa siku," ilisema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI