Kiongozi mwenye nguvu wa genge la dawa za kulevya wa Ecuador, Adolfo MacÃas Villamar amepelekwa Marekani kujibu mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya na silaha.
Anajulikana kama "Fito," alikamatwa tena mwezi Juni, karibu mwaka mmoja baada ya kutoroka katika gereza lenye ulinzi mkali alikokuwa akitumikia kifungo cha miaka 34 kwa sababu ya uhalifu.
Atafikishwa katika mahakama ya shirikisho ya Marekani siku ya Jumatatu, ambapo atakana mashtaka ya kimataifa ya ulanguzi wa dawa za kulevya na silaha, wakili wake ameiambia Reuters.
MacÃas alikuwa kiongozi wa genge la Los Choneros, ambalo linahusishwa na mashirika yenye nguvu ya uhalifu ya Mexico na Balkan. Pia anashukiwa kuamuru kuuawa kwa mgombea urais Fernando Villavicencio 2023.
Los Choneros linalaumiwa kwa kuibadilisha Ecuador kutoka nchi ya watalii hadi nchi yenye viwango vya juu vya mauaji katika eneo la Amerika.
Zaidi ya 70% ya kokeini zote zinazozalishwa ulimwenguni kwa sasa hupitia bandari za Ecuador. Nchi hiyo iko kati ya nchi ambazo ni wauzaji wakubwa wa kokeini duniani, Colombia na Peru.
Mwezi Juni, polisi walimfuatilia MacÃas hadi katika chumba cha kulala chini ya ardhi chini ya nyumba ya kifahari katika jiji la Manta. Alipelekwa La Roca, gereza lenye ulinzi mkali.
Rais wa Ecuador Daniel Noboa alivipongeza vikosi vya usalama kwa kumkamata na kusema atarejeshwa Marekani.
Mamlaka ya magereza nchini humo ilisema alitolewa gerezani huko Ecuador mapema Jumapili ili kupelekwa Marekani.
0 Comments