Header Ads Widget

IRAN YAKUBALI KUFANYA MAZUNGUMZO JUU YA NYUKLIA

 

(Kuanzia kulia) Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, David Lemmy, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Kaia Kallas, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Johann Wadeful, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, na Jean-Noël Barrot, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi amethibitisha taarifa zilizoripotiwa na na Shirika la Habari la Tasnim, kuwa nchi yake itajadiliana na nchi tatu za Ulaya, Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza kuhusu mpango wake wa nykulia.

Shirika la Habari la Tasnim, lililo karibu na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na vyombo vya usalama, liliandika siku ya Jumapili, kabla ya taarifa za Bwana Araqchi: "Mazungumzo hayo yatafanyika, lakini mashauriano yanaendelea kuhusu wakati na mahali pa mazungumzo hayo."

Saa moja baadaye, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisema, “ni lazima kwa nchi za Ulaya kufahamishwa misimamo ya Iran na kwa hakika Iran ina nguvu zaidi kuliko hapo awali katika kutafuta haki zake za baada ya vita."

Wakati huo huo shirika la habari la serikali ya nchi hiyo limemnukuu Esmail Baghai, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, akisema Istanbul imepangwa kuandaa mazungumzo hayo siku ya Ijumaa, Julai 25.

Chanzo cha kidiplomasia cha Ujerumani pia kiliiambia AFP Jumapili kwamba mataifa yenye nguvu ya Ulaya yanapanga kufanya mazungumzo mapya ya nyuklia na Iran, ambayo yatafanyika wiki hii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI