Header Ads Widget

SHULE NYINGINE MPYA YA SEKONDARI KUFUNGULIWA KESHO JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma 

KATIKA muendelezo wa ufunguzi wa shule mpya za sekondari jimbo la Musoma Vijijini kesho juni 7,2025 itafunguliwa shule ya 3 ndani ya kipindi kifupi

Shule itakayofunguliwa kesho ni ya Amali iliyopo Kata ya Nyamrandirira Kijiji cha Kasoma ambapo mgeni rasmi atakuwa mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka.

Hii ni sekondari ya tatu ya Kata hii ambayoina vijiji vitano inayokwenda kusaidia wanafunzi kujifunza elimu ya darasani na masuala ya kuwasaidia baada ya kuhitimu elimu hiyo.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo juni 7,2025 na ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo umesema maandali yote yapo tayari kwaajili ya ufunguzi wa shule hiyo.

Wananchi wa Kijiji cha Kasoma wameombwa kujitokeza kwa wingi kuanzia majira ya saa 4 asubuhi kwenye shule hiyo ili kushuhudia uzinduzi huo

Licha ya sekondari hiyo ya Amali shule nyingine ya 4 kwa mujibu wa taarifa hiyo itafunguliwa juni 9,2025 ambayo ni shule ya sekondari Muhoji ambayo ni ya pili kwenye Kata ya Muhoji yenye vijiji 4 ambapo mgeni rasmi atakuwa mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi. 

Shule ambazo tayari zimefunguliwa hivi karibuni ni shule ya sekondari Butata iliyopoKijijini Butata

ikiwa ni sekondari ya pili ya Kata ya Bukima yenye vijiji vitatu pamoja na David Massamba Memorial Secondary School iliyopo Kijijini Kurwaki Kata ya Mugango.

Aidha wananchi wameendelea kuombwa kuchangia ujenzi wa sekondari kwenye vijiji na kujitokeza kwenye uzinduzi wa shule hizo kwa tarehe zilizopangwa.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI