![]() |
Shekhe wa mkoa Kigoma Hassan Kiburwa akizungumza katika sala ya Eid Adhaa iliyofanyika viwanja vya Kawawa Ujiji mjini Kigoma |
Na Fadhili Abdallah,Kigoma.
SHEKHE wa mkoa Kigoma Hassan Iddi Kiburwa amekemea tabia ya baadhi ya watu kutoa maneno ya kuwazuia Watanzania kutogombea au kugomea kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao na kutaka wahesimu katika ya nchi ambayo inayoa uhuru wa kila mtu kuchagua au kuchaguliwa bila kuingilia na mtu mwingine.
Shekhe Kiburwa alisema hayo akitoa mawaidha ya Sala ya Eid Al Adhaa iliyofanyika kimkoa kwenye viwanja vya Kawawa Ujiji mjini Kigoma na kubainisha kuwa hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kumzuia mtu mwingine kugombea midhali havunji sharia.
Alisema kuwa maneno ya kuchochea watu kugomea kupiga kura au kugoma kugombea ni dalili za kuanza kuleta chokochoko na kuvunja Amani ya nchi hiyo ametoa wito kwa Watanzania kukemea kwa kauli moja watu wote wanaotaka kuanzisha chokochoko hizo.
![]() |
Sehemu ya waumini wa dini ya Kiislam wa mjini Kigoma waliohudhuria ibada ya Sala ya Eid iliyofanyika viwanja vya kawawa Ujiji mjini Kigoma |
Pamoja na hilo Shekhe huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa anaamini chaguzi zitasimamiwa kwa haki ili kuwapa uhuru wenye nia ya kugombea na wenye nia ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka kama ambavyo uhuru huo upo kwenye katiba ya nchi lakini hata vitabu vya dini vinaeleza uhuru huo wa kuchagua.
Awali akitoa khutuba ya Sala ya Eid Al-ad’haa Mjumbe wa baraza la Mashekhe mkoa Kigoma, Iddi Kafungo amewataka Watanzania kukemea na kufichua viashiria vyovyote vyenye lengo la kuvuruga Amani ya nchi yetu.
Shekhe Kifungo alisema kuwa ni wajibu wa Watanzania wote kumshukuru Mungu kwa Amani iliyopo ambapo amewataka kushikana kuhakikisha wanaidumisha Amani hiyo kwa kufuata misingi ya dini zao ambazo zinahimiza Amani na upendo miongoni mwao.
![]() |
Shekhe Iddi Kifungo Mjumbe Baraza la Mashekhe BAKWATA mkoa Kigoma |
0 Comments