Header Ads Widget

SHEIKH ABUBAKAR MKAMA AONGOZA DUA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU WA AMANI


Na Shomari Binda-Musoma 

SHEIKH wa Wilaya ya Musoma Abubakar Mkama ameongoza dua baada ya swala ya Eid el Hajj kuombea uchaguzi mkuu wa amani mwezi oktoba.

Dua hiyo iliyomwa kwenye Msikiti wa Taqwa uliopo Songe Kata ya Bweri manispaa ya Musoma licha ya kuombea uchaguzi wamemuombea pia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan afya njema na kuisimamia nchi.

Sheikh Abubakar amesema yanapotokea machafuko kwenye uchaguzi wanaoathirika zaidi ni watoto na wanawake hivyo ni muhimu kuombea amani.

Amesema kama viongozi wa dini wanalo jukumu la kusisitiza umuhimu wa amani na kuomba dua ili lolote lenye kuvuruga amani lisiweze kutokea.

Sheikh huyo amesema ipo mifano kwenye nchi ambazo kupitia uchaguzi kumeibuka machafuko na kusababisha adha kwa wananchi.

Amesema kila mmoja anapaswa kulinda amank iliyopo iendelee kuwepo na ujio wa uchaguzi usipelekee kuvuruga amani.

" Ndugu zangu katika imani napenda kuzungumzia umuhimu wa kuwa na amani tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo mwezi oktoba na tusikubali amani ikavurugika.

" Watoto wetu na wanawake ndio waathirika wakubwa pale amani inapovurugika tuombee uchaguzi unaokuja usivuruge amani tuliyonayo",amesema.

Aidha Sheikh huyo wa Wilaya ya Musoma amemuombea dua Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa na agya njema na kuendelea kuliongoza taifa.

Waumini katika Msikiti huo wa Taqwa wameungana na Waislam duniani kote kuswali na kusherehekea sikukuu ya Eid el Hajj baada ya kumalizika kwa ibada ya Hijah.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI